HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA CHATO YASHIRIKI KATIKA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA MAONESHO YA KIMATAIFA YA MADINI

Posted on: September 23rd, 2023

Ikiwa ni siku ya tano tangu kuanza kwa maonesho ya kimataifa ya madini, zaidi ya wananchi 300 kutoka sehemu mbalimbali wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo, kisukari, viashiria vya magonjwa ya figo pamoja na upimaji wa uwiano wa urefu na uzito katika banda la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato lililopo ndani ya viwanja vya maonesho EPZ.

Kupitia maonesho ya teknolojia ya madini mwaka 2023 yenye kauli mbiu inayosema “Matumizi ya Teknolojia Sahihi Katika Kuinua Wachimbaji Wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira, hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato imewasogezea karibu wananchi wa Mkoa huu wa Geita na mikoa mingine huduma za uchunguzi na ushauri wa lishe bora pamoja na utunzaji mazingira dhidi ya magonjwa tunayoweza kuyapata kupitia mazingira tunayoishi hasa magonjwa sugu.

Tunawakaribisha Wananchi wanaofika katika maonesho haya kufika katika banda letu kupata fursa ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa hayo bila malipo.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.