WAFANYAKAZI HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA CHATO WASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2025 MKOA WA GEITA.

Posted on: May 1st, 2025


Wafanyakazi wa Afya na wanachama wa TUGHE tawi la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato wameshiriki katika matembezi ya pamoja na wafanyakazi mbalimbali kutoka mkoa wa Geita kama sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo huadhimishwa tarehe 1 Mei kila mwaka.

Matembezi hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Kalangalala vilivyopo manispaa ya mji wa Geita, Mkoa wa Geita. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita , Mheshimiwa Martine Shigella.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mkuu wa Mkoa amewashukuru Viongozi wa taasisi za umma na binafsi kwa kuendelea kutambua na kuboresha maslahi ya watumishi jambo ambalo limepunguza malalamiko na amesisitiza nidhamu kazini na uwajibikaji Kama msingi wa utoaji huduma bora kwa jamii.

“Ni wajibu wa kila mfanyakazi kuwajibika, kulinda na kutetea haki za wananchi tunaowahudumia. Tunapokuwa katika kazi zetu, tunabeba taswira ya serikali, hivyo ni muhimu tuendelee kufanya kazi kwa bidii na uaminifu,” alisema Mhe.Shigella

Maadhimisho ya kitaifa mwaka huu yamefanyika mkoani Singida, yakiwa na kaulimbiu: “Uchaguzi Mkuu wa 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali na Kuthamini Haki ya Maslahi ya Wafanyakazi.”

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.