HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA - CHATO YAPOKEA BILIONI 18 ZA VIFAA TIBA

Posted on: October 14th, 2022

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato imepokea bilioni 18 kwa ajili ya vifaa tiba vya kisasa kama CT - scan, MRI, Thioroscope na ECHO kwa ajili ya uboreshaji huduma za afya kanda ya Ziwa.

Waziri Ummy amebainisha kauli hiyo leo Wilayani Chato mkoani Geita wakati akikagua maandalizi ya kuweza kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani anayetarajia kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato siku ya Jumamosi Tarehe 15 Oktoba, Mwaka huu.

Akizungumza Mhe. Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Hospitali hii itahudumia wagonjwa kutoka mikoa ya Jirani ili kupunguza mzigo mkubwa kwa Hospitali ya Bugando na Wizara ya Afya wataipa kipaumbele kwa kuhakikisha kila kinacho hitajika katika hospitali kinapatikana kwa haraka kwa umuhimu wa hospitali hii.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.