Tangazo, Huduma Ya Mifupa kutolewa na madaktari bingwa katika hospitali ya kanda ya rufaa chato
Posted on: March 15th, 2022Madaktari bingwa wa mifupa wa hospitali ya kanda ya rufaa chato wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya rufaa ya Dodoma kuanzia leo tarehe 15/03/2022 kwa muda wa siku kumi watakuwa katika hospitali ya Kanda ya Rufaa Chato wakitoa huduma za matatizo ya mifupa iliyovunjika au inayohitaji upasuji.
Hivyo wananchi wote wa mikoa/maeneo jirani na wakutoka sehemu mbalimbali mnakaribishwa kwa ajili ya kupata huduma hiyo katika hospitali ya kanda ya rufaa Chato inayopatikana kwa muda wa masaa 24.
