kamati ya siasa ya mkoa wa geita yatembelea hospitali ya rufaa ya kanda chato
Posted on: March 19th, 2022Kamati ya siasa ya mkoa wa Geita imempongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan rais wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita kuendelea kutoa pesa za kukamilisha mradi wa ujenzi wa Hospitali rufaa ya kanda Chato na kutenga pesa kutoka fedha za IMF kwa ajili ya Ununuzi wa Vifaa tiba mfano CT Scan, MRI, na vingine. na wameshauri jitihada mbalimbali za kutangaza huduma zitolewazo katika hospitali zifanyike ili wananchi waweze kuzifahamu na kufika kupata huduma za matibabu hospitalini hapa.
Hayo yamesemwa leo tarehe 19 marchi 2022 na wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Geita ikiongozwa na katibu wa CCM mkoa wa Geita Mhe. Alexandrina Katabi na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha Mkupasi wakati wa kutembelea miradi.
Katibu wa CCM mkoa wa Geita Mhe. Alexandrina Katabi amesema kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika hospitali hiyo amewapongeza watumishi kwa kazi wanayoitoa kwa wananchi na kuwasihi wasikate tamaa kwa kuwa kazi wanayoifanya ni kazi ya wito inayochukua muda mwingi kwa mtumishi kuwa kazini na wakati mwingine kulazimika kuicha familia yake kuwahudumia wananchi.
