KIKAO CHA MAZUNGUMZO YA UANZISHWAJI WA CHUO CHA AFYA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA CHATO

Posted on: August 18th, 2023

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato leo Agosti 18 2023, umepokea wageni kutoka @wizara_afyatz na @mwachas_bugando na kufanya mazungumzo ambayo yana lengo la kuboresha na kuiendeleza hospitali hii ili kufikia lengo thabiti katika utoaji wa huduma za Afya kwa Wananchi.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika hospitalini hapa Dkt.Hyasinta Jaka, Mkuu wa chuo hicho amesema, "mazungumzo haya ni imani yetu kwamba yanaenda kuleta tija katika utoaji wa huduma za afya hasa kwa Wananchi wa Mkoa huu wa Geita na Kanda ya ziwa kwa ujumla.Huduma zinaendelea kuimarika na tutaimarika zaidi hasa katika kuongeza Nguvu kazi kwa hospitali hii ambayo Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt.@samia_suluhu_hassan imelenga kuijenga na kuimarisha huduma zake Kama vile ilivyokusudia"

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato Dkt.Brian C. Mawalla, amewashukuru Viongozi hawa kwa kuitembelea na kufika katika hospitali hii na kuwaomba kuendeleza Ushirikiano huu kwa maslahi ya Wananchi wetu ambao tumejipanga kuwahudumia na kuokoa maisha yao.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.