KIKAO CHA MPANGO MKAKATI WA USHIRIKIANO KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KATI YA HOSPITALI NA SHIRIKA LA GLOBAL HEALTH CARE

Posted on: August 22nd, 2023

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato imepokea wageni kutoka Global Health Care ambao wanafanya kazi zao katika mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Tanzania-Uganda lenye urefu wa kilomita 1400,linalotarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2025. Mkoa wa Geita (ikiwemo Wilaya ya Chato) ni kati ya mikoa nane ya Tanzania ambapo mradi huu unapita.

Lengo la kuitembelea hospitali hii ni kuweka mpango mkakati wa Ushirikiano kati yao na hospitali wa kutoa huduma za afya katika kipindi cha ujenzi huo,ambapo wametembelea na kuona miundombinu,vifaa tiba na mashine za kisasa zilizofungwa katika hospitali hii pamoja na hali ya utoaji huduma.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya hospitali,Pascaline Wolfermann kutoka Global Health care ,amesema amefurahishwa na ujenzi wa Hospitali hii ikiwa ni pamoja na juhudi za Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Kuhakikisha inaweka miundombinu,vifaa tiba,mashine za kisasa hasa CT Scan na MRI ambazo zitasaidia sana katika uchunguzi na matibabu hivyo kuokoa maisha ya Wananchi na endapo watumishi katika mradi huo watapata changamoto.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.