MADAKTARI BINGWA HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA YA CHATO WAFANYA UPASUAJI KWA MTOTO ALIYEZALIWA BILA KUWA NA SEHEMU YA KUTOLEA HAJA KUBWA
Posted on: February 19th, 2022Hospitali ya Kanda ya Rufaa Chato, imeweza kufanya upasuaji kwa mtoto aliyezaliwa bila kuwa na sehemu ya kutolea haja kubwa. Upasuaji huu bobezi umefanywa na madaktari bingwa wa hospitali hii ya Kanda ya Rufaa ya Chato wakiwa wamefanikisha kumsaidia mtoto huyu.
Hivyo kwa wale wenye matatizo kama haya na mengine wanakaribishwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa Chato kwa ajili ya kupatiwa Uchunguzi na matibabu yakinifu kwani inamadaktari bingwa na bobezi wa kutosha.
