MADAKTARI BINGWA WA UPASUAJI NA WATAALAMU WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA CHATO WAMEENDESHA ZOEZI LA UPASUAJI NYANG'HWALE
Posted on: November 2nd, 2023Wataalamu na Madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Nyang'hwale, leo 02 Novemba, 2023 wameendelea na zoezi la utoaji huduma za afya kwa wananchi ndani ya Wilaya hii, ambapo zaidi ya wananchi 20 kati ya wale waliohudumiwa wamefanyiwa upasuaji mkubwa na mdogo.
Zoezi la utoaji huduma hizi katika kambi ya siku tano lilianza tarehe 30 Octoba, 2023 na linategemewa kuhitimishwa kesho tarehe 3 Novemba, 2023 huku zaidi ya wananchi 900 wakiwa wamehudumiwa na wengine kupewa rufaa kwa ajili ya matibabu zaidi na uangalizi wa madaktari kulingana na hali zao za kiafya.