MAFUNZO JUU YA KUHUDUMIA WAGONJWA WA DHARULA
Posted on: September 2nd, 2023Wizara ya Afya katika Kuhakikisha inaendelea kuimarisha afua ya utoaji huduma za tiba kwa magonjwa ya mlipuko ikiwemo UVIKO-19, imeendelea kuwajengea uwezo watoa Huduma za Afya kwa kuwapatia mafunzo kulingana na miongozo iliyowekwa na Wizara.
Mafunzo haya yanalenga kuwawezesha kupata uelewa na kuwa tayari kutoa mafunzo kwa Watumishi wengine ndani na nje ya kituo chetu cha kutolea huduma.
Katika kutekeleza azma hii, Wizara ya Afya kupitia kamati ndogo ya matibabu (case management), imeendelea kufanya tathmini na kutoa mafunzo kwa Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato ambayo yanalenga kuwafanya kuwa tayari kuwahudumia Wagonjwa wa dharula katika maeneo yao ya kazi ambayo yamefanyika hospitalini hapa.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo haya, Ndugu Mary Archson Makata kutoka Wizara ya Afya ametoa wito kwa Watumishi waliopata mafunzo kuitumia elimu hii kuboresha huduma za dharula na ameishukuru hospitali kukubali na kuitikia wito wa kushiriki mafunzo haya muhimu yenye lengo la kuokoa maisha ya Watanzania.