MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA MWENZA KUTOKA WORLD RENEW ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA CHATO

Posted on: October 26th, 2023

Mkurugenzi Mkuu wa shirika mwenza kutoka World Renew akiongozana na mratibu wa mama na mtoto Ndugu Freddy Ulembo, Katibu wa Afya Hospitali ya Wilaya ya Chato Ndugu Shamsi Abdallah, Afisa lishe Wilaya Ndugu Renatus Komba na wajumbe wengine, wameitembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato na kufanya mazungumzo na uongozi wa Hospitali.

Ni katika utekelezaji wa mradi unaolenga kuboresha afya ya lishe ya mama na mtoto katika Wilaya ya Chato kwa vijiji 12 ambao umeanza kutekelezwa mwaka 2022 na utekelezaji huu unatarajiwa kuisha mwaka 2026.

Mara baada ya kikao kifupi,wajumbe hawa wamekabidhi maziwa ya watoto ambayo yatawasaidia watoto wachanga ambao hukosa maziwa ya mama kutokana na changamoto mbalimbali ambapo maziwa haya hutumika kama mbadala wa maziwa ya mama kwa mtoto ili aweze kukua kiafya.

Naye Afisa lishe Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato Ndugu Haule John mara baada ya kukabidhiwa maziwa hayo, amewashukuru wajumbe hawa kwa kujitoa kuimarisha afya lishe kwani kwa kufanya hivyo wameokoa maisha ya watoto ambao huzaliwa na kukosa maziwa ya mama ambayo Yana virutubisho muhimu kusaidia ukuaji wao.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.