JENGO LA RUFAA
Posted on: November 19th, 2020Kamati ya siasa ya mkoa wa Geita imepongeza uamuzi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuamua kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda iliyopo Chato na wameshauri jitihada mbalimbali za kuitangaza hospitali hiyo zifanyike ili wananchi waweze kuifahamu na kwenda kupata huduma za matibabu hospitalini hapo.
