TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
Posted on: December 6th, 2024Majukumu ya Kitengo cha Teknolojia ya Habari( TEHAMA)
- Kutayarisha mpango Mkakati wa kuhusu teknolojia ya habari na mawasiliano, Miongozo na taratibu kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
- Kuishauri Menejimenti ya halmashauri ya masuala yanayohusiana na sera zinazohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano na utekelezaji wa dhana ya serikali mtandao.
- Kuishauri Menejimenti ya halmashauri juu ya masuala yanayohusiana na sera, miongozo na taratibu zinazohusiana na takwimu.
- Kusimamia maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano na utekelezaji wake kwa ajili ya halmashauri.
- Kutoa na kuratibu msaada wa teknolojia ya habari kwa menejimenti ya halmashauri.
- Kutathimini, kuboresha na kusimamia teknolojia ya habari na mawasiliano na usimamizi wa mifumo ya taarifa/habari iliyosimikwa/iliyowekwa kwenye halmashauri.
- Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo juu ya usimamizi wa mifumo ya taarifa na teknolojia ya habari na mawasiliano na kuandaa mpango wa kujenga uwezo
- Kufanya tathimini ya hatari/hasara zinazohusiana na miundombinu ya teknolojia ya habari na mawasiliano na mfumo wa usimamizi wa taarifa na namna ya kuthibiti.
- Kuandaa sera ya Tehama
- Kusimamia Tovuti ya Halmashauri