HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII
Posted on: October 10th, 2024- Kufanya uchunguzi/ tathmini kwa wagonjwa wenye matatizo ya kijamii au kisaikolojia [ social and psycho-social problem) ili kujua jinsi ya kushughulikia
- Kutoa ushauri kwa wagonjwa na/ au ndugu wa wagonjwa waliobainika kua na matatizo ya kijamii au kisaikolojia( social and psychosocial problem).
- Kutoa msamaha wa matibabu kwa makundi wa magonjwa yaliyosamehewa kwa mujibu wa sera ya afya na wasiokua na uwezo kiuchumi.
- Kufanya social ward round ili kubaini na kutoa huduma kwa wagonjwa wenye shida za kisocial au kisaikolojia, mfano pre couselling kabla ya kukatwa kiungo au operation yoyote.
- Rufaa yaani kuwasafirisha kwenda hospitali husika wale wasiojiweza na kuwaunganisha na ndugu zao (family re-unification) wale waliotelekezwa na ndugu zao na wenye migogoro ya kifamilia.
- Kufanya huduma shufaa (palliative care) kwa wagonjwa wenye magonjwa sugu au ya muda mrefu mfano cancer, HIV/AIDs n.k.
- Kushirikiana na watoa huduma wengine ili kuhakikisha mgonjwa anapata huduma ya matibabu kwa ujumla wake.
- Kutoa elimu ya msingi (basic education) kwa wagonjwa ndugu ili kuwapa uelewa mzuri juu ya ugonjwa husika na kujua jinsi ya kuuchughulikia kwa ufaniisi.
- Kushughulikia mashauri yote yatokanayo na manyanyaso ya kijinsia ( Gender Based Violence –GBV)
- Kuhudhuria clinic za afya ya akili na CTC ili kubaini na kutoa huduma kwa wagonjwa wenye kuhitaji huduma za kiustawi
- Nb. Ukibaini mgonjwa yeyote mwenye tatizo lolote la kijamii au kisaikolojia, tafadhali muite social worker amuone. Kinyume na hapo ni kumkosea haki yake kimsingi.