HUDUMA ZA KITABIBU
Posted on: September 12th, 2024Huduma kwa Wagonjwa wa Ndani
- Kupitia taratibu za uchunguzi wa kitabibu utambuzi wa magonjwa hufanyika na kuhakikisha matibabu sahihi hutolewa kwa kila mgonjwa.
- Mzunguko wa kuona wagonjwa Wodini Hufanywa kila siku asubuhi.
- Kushauriana na Idara nyingine kwa ajili ya utambuzu wajumla na matibabu ya magonjwa yenye muingiliano wa idara Zaidi ya moja.
Huduma kwa Wagonjwa wa Nje
Idara hutoa huduma za kawaida za magonjwa ya ndani na huduma mbalimbali za kibingwa kwa wagonjwa wanaohudhuria kliniki zetu. Kliniki hizi ni kama zifuatazo:
- Kliniki ya kawaida ya magonjwa ya ndani: Huduma ya Matibabu na kufuatilia maendeleo ya matibabu kwa wagonjwa walioruhusiwa na kwa magonjwa tofauti yasiyo ya dharura yenye kuhitaji kulazwa. Mfano: Presha ya kupanda, Baada ya Kiharusi, vidonda vya tumbo, Upungufu wa damu n.k. Hufanya kazi kila siku
- Kliniki ya Sukari: Huduma ya Matibabu na kufuatilia maendeleo ya matibabu kwa wagonjwa wa Kisukari. Hufanya kazi kwa siku zote za kazi katika wiki Jumatatu hadi Ijumaa.
- CTC: mahususi kwaajili ya tiba na kujali wateja/wagonjwa na familia zilizoathirika na ugonjwa wa Ukimwi. Hufanya kazi kwa siku zote za kazi katika wiki Jumatatu hadi Ijumaa.