MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, 2025.
Posted on: March 2nd, 2025Baadhi ya wanawake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato mapema Machi 02, 2025, walishiriki Kongamano la Kanda ya Ziwa lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ushirombo Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima ambaye aliwaasa wanawake kutumia vyema fursa za mikopo inayotolewa na Halmashauri pamoja na Taasisi nyingine za kifedha kama mabenki na kuonyesha uaminifu katika urejeshaji wa fedha hizo. Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake kitaifa yanatarajiwa kufanyika Machi 8, 2025 mkoani Arusha.
