TUGHE HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA CHATO WATEMBELEA KITUO CHA KULEA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU CHATO.
Posted on: April 12th, 2025Viongozi wawakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato leo Aprili 12, 2025 wametembelea kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mennonite kilichopo Chato kwa lengo la kuwashika mkono ikiwa ni sehemu yao ya kufanya matendo ya huruma hasa katika kipindi hiki cha mfungo wa kwaresma.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea viongozi hawa, Bwana. Zephaline Charles Mratibu katika kituo hiki, amewashukuru wanachama hawa kwa kuguswa na maisha ya Watoto hawa na kusema;
“Tendo hili ni tendo la kiimani na huruma kwa Watoto hawa kwani wanatuhitaji kuwalinda na kuwawezesha kielimu, kiroho na kuwatengenezea kesho yao. Tunahitaji kuwalinda kiroho na imani huku tukiwapa elimu wapate mwangaza na maarifa ya kuwasaidia katika Maisha yao.Tuendelee kuwasaidia kwa ajili ya kesho yao ya baadae na Mungu awaongezee pale mlipotoa.
Naye bi. Yunis O. Kiiza akizungumza kwa niaba ya wanachama, amesema
“Chama kimeandaa zawadi na mahitaji haya kwa Watoto hawa ili kuwasiadia na kuwalinda katika safari yao ya elimu waweze kusoma na kwa kuwa ni mfungo wa kwaresma, basi kama chama tumeona ni wakati sahihi na sisi kuungana na Watoto hawa kwa chochote kwani wanahitaji faraja na tutaendelea kuwaunga mkono kwa chochote tutakachokuwa nacho kwa ajili yao.
