MAFUNZO YA UTUMISHI NA NAMNA BORA YA UTOAJI HUDUMA YA AFYA ILIYO BORA

Posted on: February 12th, 2023

Watumishi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato wamepokea mafunzo elekezi ya kiutumishi ikiwa ni pamoja na mafunzo ya namna bora ya utoaji huduma sahihi na elekezi kwa wananchi wote wanaofika katika hospitali hii kupata huduma za afya.

Mafunzo haya yanalenga kuwafundisha na kuwaongezea ujuzi watoa huduma ikiwa ni pamoja na kuwapokea na kuwapatia huduma wananchi wote kwa usawa ambayo ni sehemu ya kuimarisha utoaji huduma unaofuata miongozi iliyowekwa na serikali ili kuhakikisha wananchi wananufaika na huduma za afya zinazowazunguka.

Mafunzo haya yamefanyika siku tatu, kuanzia tarehe 8 februari, 2023 hadi 10 februari, 2023. yameratibiwa na wataalam wa masuala ya afya na utumishi ambao ni; afisa utumishi hospitali ya rufaa ya kanda-chato ndugu Elly R. Aketch, Masudi eliah biteyamanga (afisa tawala mkuu mstaafu) na ndugu Paul samwel yoseph( afisa tawala mwandamizi).

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.