RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA-CHATO

Posted on: October 15th, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aahidi Hospitali Rufaa ya Kanda - Chato kujengwa kama ilivyokusudiwa

Rais Samia Ametoa ahadi hio leo katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda - Chato

"Hospitali hii mpaka sasa majengo matano yapo tayari Niwahakikishie tutaijenga kama ilivyokusudiwa, wataalamu wakutosha wamesha letwa na tutaendelea kuwaleta" Amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia amewataka Wana Chato kujitokeza kwa wingi kujiunga na Bima ya Afya kwa wote pindi itakapoanza kufanya kazi ili kupata Huduma bora za afya katika Hospitali hiyo kwa gharama zilizo ndani ya Bima hiyo.

"Niwaombe sana tutakapo kuja na mfumo wa Bima ya Afya kwa wote, wote tukanunue bima ni kupitia bima hizo tunaweza tukaboresha zaidi huduma hizi za afya" Amesema Rais Samia

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.