SIKU YA WAUUGUZI DUNIANI 12 MEI 2022

Posted on: May 12th, 2022

Serikali inatambua na kuthamini umuhimu na mchango mkubwa wa wauguzi katika jamii na kwamba ndio kada ya afya ambayo watumishi wake wanatumia muda mrefu kuhudumia mgonjwa hivyo imejipanga kutatua changamoto mbalimbali zinazoigusa kada hiyo. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mh. Dorothy Gwajima akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa katika kilele cha siku ya wauguzi duniani kilichofanyika Mei 12 katika viwanja vya Chuo Cha Ushirika (MUCO) Mkoani Kilimanjaro.

“Nimesikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo suala la kuchelewa kwa muundo wa utumishi wa maendeleo ya kada ya uuguzi na ukunga na kutotambuliwa wauguzi wenye stashahada ya juu na wenye shahada ya uzamili (Wauguzi Bingwa), kutozingatia kianzia cha mshahara kwa wauguzi wenye shahada ya kwanza ukilinganisha na muda wao wa masomo,  hivyo basi naagiza Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora pamoja na Waziri wa Afya kupata ufumbuzi wa jambo hili kwa haraka”amesema hayowakati akisoma hotuba ya Waziri Mkuu.

Wauuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda- Chato wakiungana na wauguzi wote duniani katika kuazimisha siku hii ya wauguzi waliweza kufanya maandamano kwa umoja wao wakiwa wamevaa sare ya Hospitali ya rufaa ya Kanda Chato na kutoa chochote kitu kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wodi za hospitali hii.

Siku ya uuguzi duniani huadhimishwa kila tarehe 12 Mei ambapo mwaka huu Tanzania imefanyika katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi (MUCO) na ilibeba kauli mbiu isemayo “wauguzi: sauti inayoongoza, wekeza kwenye uuguzi na heshimu haki kwa manufaa ya afya kwa wote”, Imehudhuriwa na wauguzi kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwemo wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda- Chato(CZRH).

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.