UZINDUZI WA KLINIKI YA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO WAKATI WA UFUNGUZI WA KAMBI MAALUMU YA MATIBABU YA MOYO INAYOFANYIKA KATI YA TAREHE 31 OCTOBA HADI TAREHE 4 NOVEMBA 2022

Posted on: November 1st, 2022

Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe.Martha Mkupasi leo Tarehe 1 Novemba 2022 amekata utepe kuashiria kuzindua kliniki ya Uchunguzi wa magonjwa ya Moyo wakati wa ufunguzi wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo inayofanywa na Madaktari wa Jakaya Kikwete wakishirikiana na wenzao wa Hospitari ya Rufaa ya Kanda Chato.

Katika hafla hiyo fupi,Mhe. Martha Mkupasi ameishukuru serikali na Wizara ya Afya kwa kufanikisha kuwepo kwa Hospitali hii na kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Geita na Mikoa jirani kuhudhuria katika matibabu haya yaliyosogezwa karibu ndani ya Kanda ya ziwa huku ikiwapunguzia gharama walio wengi kuzifuata huduma hizi mkoa wa mbali ambao ni Dar es Salaam.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.